Kitengo cha Dini kinagawa unga katika mitaa ya mafakiri ndani ya mji mtukufu wa Karbala.

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kugawa unga kwa mafakiri na watu wenye kipato kidogo ndani ya mji mtukufu wa Karbala, baada ya tangazo la marufuku ya kutembea barabarani.

Rais wa kitengo hicho Shekh Swalahu Karbalai amesema kua: “Hii ni sehemu ya harakati nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kupunguza japo kidogo shida za familia za mafakiri hapa Karbala, tumeanza kugawa unga kwa familia hizo baada ya serikali ya mkoa kupiga marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Korona”.

Karbalai akasisitiza kua: “Jambo hili ni la kibinaadamu linaweza kufanywa na mtu yeyote sawa awe anatoka katika Atabatu Abbasiyya au kwingineko, ni sehemu ya kuendelea kusaidiana kujilinda na hatari hii pamoja na kugawana riziki tuliyo pewa na Mwenyezi Mungu, pamoja na udogo wa misaada hii lakini inasaidia kupunguza makali ya maisha kwa familia hizo katika kipindi hiki kigumu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: