Kikosi cha kujilinda na majanga chini ya kamati maalum iliyo undwa na idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza kazi ya kupuliza dawa barabara na nyumba za makazi za Abbasi (a.s), kazi hiyo inafanywa kwa ajili ya kujilinda na virusi vya Korona na kuwalinda wakazi wa nyumba hizo.
Tumeongea na mkuu wa opresheni hiyo Ustadh Hassan Ali Abdulhussein amesema kua: “Kikosi cha kujilinda na majanga chini ya kamati maalum iliyo undwa na Atabatu Abbasiyya, kimeanza kupuliza dawa kwenye nyumba za makazi za Abbasi (a.s), chini ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, kazi hiyo imehusisha upuliziaji wa dawa katika mji mkongwe na maeneo yanayo zunguka Ataba hadi pembezoni mwa mji, kwa kutumia dawa na vifaa walivyo pewa na shirika la Khairul-Juud, kazi hiyo inafanywa kwa kufuata maelekezo ya wizara ya afya ya Iraq na shirika la afya la umoja wa mataifa”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imesha chukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kazi hiyo, pamoja na kufanyia kazi maelekezo yote yanayo tolewa na idara za afya ndani ya Ataba, katika vitengo vyake na katika mji mkongwe.