Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi siku ya Alkhamisi (19/03/2020m) sawa na (23 Rajabu 1441h) amekutana na viongozi wa Hashdi zilizo undwa na Ataba, ambao ni: (Sayyid Hamiid Yaasiri - kiongozi wa Liwaau Answaru Marjaiyya (l/44), Shekh Twahiru Khaqaani - kiongozi wa kikosi cha Imamu Ali (Liwaau/2), Luleni Ali Hamdani – kamanda wa Liwaau Ali Akbaru (Liwaau/11), Shekh Maitham Zaidi – kiongozi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji (Liwaau/26)), kujadili mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa na maendeleo ya vikosi hivyo.
Katika kikao hicho Mheshimiwa amesisitiza umuhimu wa vikosi vyote vya Hashdi Shaábi kufanya kazi kwa uzalendo, hilo sio jambo jipya bali ni jambo la kawaida katika kila nchi.
Akaongeza kua: “Watu waliopigana na kuleta ushindi wana haki ya kufanya kazi za kiidara, kwani wao waliitikia wito wa fatwa iliyo tolewa na bwana wa fatwa katika nchi ya fatwa Iraq ambayo inasubiri mambo mengi kutoka kwetu”.
Akabainisha kua: “Walivumilia matatizo makubwa wakati wa vita, wakapambana na mitihani mingi, ambaye yupo pamoja nao anapewa haki zote na asiyekua pamoja nao ananyimwa haki zote, jambo ambalo sio la kimaadili, bado mambo hayo yapo kwa baadhi ya watu, baya zaidi wanamzushia uwongo Marjaa mtukufu wetu na mtukufu wao, watu kama hao unaweza kuamiliana nao vipi”?
Akafafanua kua: “Nyie hamumfanyii zuhudi yeyote, atakaewafanyia zuhudi basi nyie mtakua na zuhudi zaidi yake”.
Wakahitimisha kikao kwa kuonyesha kazi wanazofanya katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona yanayo tishia wananchi, Mheshimiwa akasisitiza ulazima wa kuheshimu na kufanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na taasisi za afya pamoja na jeshi la wananchi kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivyo.