Jengo la kibiashara Al-Afaal linachukua hatua za kujilinda na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Jengo la kibiashara Al-Afaaf chini ya Atabatu Abbasiyya limechukua hatua za kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona kama ilivyo elekezwa na kamati maalum ya kujikinga na majanga, kwa kufanya kazi ya kupuliza dawa kwenye jengo hilo pamoja na kutoa elimu na maelekezo ya kujikinga kwa wateja.

Watumishi wa usafi katika jengo hilo wameongeza juhudi katika kazi zao, wanafanya kazi kubwa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ukizingatia kua jengo hilo linatembelewa na watu wengi zaidi, ni jukumu lao kulinda usalama wa watumishi na watu wanaokuja kununua mahitaji yao.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya usafi bwana Aamiri Mahadi amesema kua: “Kufanya usafi katika jengo hili kila siku ni jambo la kawaida, lakini baada ya tishio la maambukizi ya virusi vya Korona usafi umeimarishwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kuweka vifungashio maalum, kupuliza dawa kila wakati, pamoja na kutoe elimu ya kujikinga na virusi vya Korona kwa wateja, sambamba na kuhakikisha wateja wananawa mikono au kufaa soksi za mikononi kabla ya kuingia katika jengo hili kwa ajili ya usalama wao”.

Kumbuka kua wafanya kazi wa jengo la kibiashara Al-Afaaf wanatekeleza kwa ukamilifu maagizo ya idara ya afya na yale ya kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya Korona, sambamba na kupewa kila kinacho hitajika kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: