Mwezi ishirini na tano Rajabu waumini hukumbuka kifo cha Imamu Alkadhim (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya kesho mwezi ishirini na tano Rajabu umma wa kiislamu unakumbuka kifo cha Imamu wa saba na mlango wa waombaji Imamu Alkadhim (a.s).

Imamu Alkadhim (a.s) alikua na elimu sawa na baba zake, wao ndio waendelezaji wa ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliishi zama muhimu sana katika uhai wa uislamu, zama ambazo zilidhihiri madhehebu nyingi za kifikra na kifalsafa, na kuwa zama hatari katika historia ya kiislamu.

Sehemu kubwa ya uhai wake aliishi ndani ya gereza zenye giza, alikua anahamishwa gereza moja hadi lingine, alitumia nafasi hiyo kufanya ibada zaidi, alitumia upweke wa gerezani kumtaja Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwake.

Pamoja na watawala wa Abbasiyya kumfanyia dhulma nyingi na unyanyasaji lakini hawakufanikiwa kumshinda (a.s), hawakua na chaguo lingine zaidi ya kumuuwa kwa sumu (a.s) na kumaliza uhai wake katika siku ya mwezi 25 Rajabu mwaka wa 183h, akazikwa katika mji wa Bagdad sehemu ya Karkha, amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayo fufuliwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: