Wanachama wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wamekamilisha kupuliza dawa katika barabara za mji wa Karbala

Maoni katika picha
Wanachama wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wamemaliza kazi ya kupuliza dawa katika barabara za mji wa Karbala, wanachama hao wameshiriki katika opresheni kubwa ya kupuliza dawa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala.

Maeneo yaliyo puliziwa dawa ni: Mtaa wa Jaair, Quntwara Salaam, barabara ya Mudarrisiy, Shabanaat, Hauli Jaair, na eneo la Fariihah.

Mzungumzaji wa kikosi amesema: Kazi inaendelea siku ya nne mfululizo kwa kushirikiana na kamati maalum ya kupambana na majanga pamoja na jeshi la wananchi, huku baadhi ya wananchi wakipewa vifaa vya kujikinga na maambukizi.

Kumbuka kua jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala kwa kushirikiana na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wanaendesha opresheni kubwa ya kupuliza dawa sehemu zote na Mkoa wa Karbala, pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na kutekeleza agizo la kutotembea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: