Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu: Sheria tukufu haijaturuhusu kuangamiza nafsi zetu

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi siku ya Ijumaa (24 Rajabu 1441h) sawa na (20 Machi 2020m) katika ujumbe aliotoa kwenye luninga (tv) amesema kua; sharia tukufu haijaturuhusu kuangamiza nafsi zetu, bali inatutaka tuzilinde.

Kutokana na itikadi yetu, Mwenyezi Mungu anasema: (Sema hatutapatwa na jambo ispokua alilotuandikia Mwenyezi Mungu), Muumini wakati woto huwa anautulivu, huo ndio uhusiano kati ya mja na Mola wake, kama ilivyo pokewa katika baadhi za dua (Kheri yako hushuka kwetu na shari zetu hupanda kwako), tunaamiliana na Mwenyezi Mungu mtukufu, naye ndio kilele cha kheri na rehema, kila kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu mja anatakiwa akiheshimu na kukinyenyekea”.

Akaongeza kua: “Kwa hiyo mtu mwenye Imani wakati wote anatakiwa awe mpole na mtulivu, mwanaadamu hubadilika kutoka hali moja hadi nyingine”.

Akafafanua kua: “Lakini mwanaadamu anatakiwa alinde nafsi yake, sheria tukufu haituruhusu kuangamiza nafsi zetu, bali inatutaka tuzilinde, kwa hiyo hata katika jambo hili –nasema- hatutakiwi kudharau virusi hivi (Korona), tuchukue tahadhari zote kuzilinda nafsi zetu –Allah atuepushie- mwanaadamu hawajibiki kulinda nafsi yake peke yake, bali anawajibika kulinda na nafsi za watu wengine vilevile”.

Akaendelea kusema: “Maelekezo yanayo tolewa na idara za afya lazima tuyafanyie kazi, kwa lengo la kulinda nafsi zetu na nafsi za watu wengine, jambo hilo halipingani na itikadi yetu, upande mmoja mtu mwenye Imani anaamini kila kitu kinatoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, lakini wakati huohuo Dini inamtaka alinde nafsi yake, kila mtu anatakiwa atumie vifaa vya kujikinga na maambukizi ya maradhi haya hatari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: