Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu: Kujikinga na maambukizi ni lazima hadi tumalize kipindi cha khofu

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi siku ya Ijumaa (24 Rajabu 1441h) sawa na (20 Machi 2020m) katika ujumbe aliotoa kwenye luninga (tv), amesema kua; kujikinga na maambukizi ni lazima hadi tumalize kipindi cha Khofu.

Akaongeza kua: “Hatutakiwi kua na khofu wala dharau, tunatakiwa kuwa na msimamo wa kati na kumuomba Mwenyezi Mungu atuepushie kila baya”.

Akasema kua: “Tunatoa pongezi kubwa kwa madaktari na wauguzi wanaofanya kazi usiku na mchana kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, wakati huohuo mgonjwa anatakiwa afanyiwe kila kitu kitakacho mfanya ajihisi kua na amani, na kupata matumaini ya kuokoka kwenye janga hilo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: