Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi siku ya Ijumaa (24 Rajabu 1441h) sawa na (20 Machi 2020m), katika ujumbe aliotoa kwenye luninga (tv), amehimiza ulazima wa kulinda nafsi na kufuata maelekezo ya idara ya afya.
Akaongeza kua: “Ni wajibu kwa kila mwananchi alinde nafsi yake, na wala asijiangamize mwenyewe, sambamba na kufanyia kazi maelekezo ya idara ya afya, tusipo fanya hivyo yanaweza kutokea matatizo makubwa yasiyo wezekana”.
Akabainisha kua: “Kila baada ya muda tunasikia takwimu za maradhi haya, baadhi ya nchi zinazodai kua zimeendelea katika maswala ya tiba maradhi haya yamesambaa kwa kasi, bado maradhi haya yanaendelea kusambaa, idara za afya zimetoa maelekezo ya kujilinda na virusi vya Korona kulingana na hali ya uwezo wa kila taifa”.