Idara ya mambo ya nje katika Atabatu Abbasiyya, inashirikiana na kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya Korona iliyo undwa na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo inafanya kazi ya kupuliza dawa katika mji mkongwe na maeneo mengine ya mji wa Karbala, tayali wamesha puliza dawa sehemu mbalimbali za mji mtukufu wa Karbala.
Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Dhiyaau Hasanawi amesema kua: “Kazi ya kupuliza dawa imehusisha maeneo ya mtaa wa Nasru, Atwibbaau, Binaau Jaahiz pamoja na sehemu zingine mbalimbali, tunatarajia kuendelea katika mtaa wa Askariy, Abbasi na Zaharaa sambamba na vituo vya polisi”.
Opresheni hiyo inatokana na ujumbe wa Marjaa Dini mkuu unao himiza kufuata maelekezo ya idara ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona katika mji wa Karbala.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake na taasisi zake, inafanya harakati mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.