Katika uwanja wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s)

Maoni katika picha
Imamu Mussa bun Jafari (a.s) ambae tunakumbuka kifo chake katika siku hizi, ni Imamu wa saba baada ya Mtume (s.a.w.w) katika kizazi chake kitakasifu, watu ambao Mtume (s.a.w.w) amewalinganisha na kitabu cha Mwenyezi Mungu, akawafanya kua kiigizo chema na meli ya uongofu na usalama wa walimwengu.. hakika wao wanatokana na nyumba ya Utume na wahay.

Tunataja baadhi ya sifa za Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Jina na nasaba yake: Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Laqabu zake mashuhuri: Kaadhim, Haliim, Twaahir, Tuhur, Abdu-Swaaleh, Baabul-Hawaaij.

Kiniya zake: Abu Ibrahim, Abul-Hassan wa kwanza, Abul-Hassan aliyepita.

Baba yake: Imamu Jafari Swadiq (a.s).

mama yake: Hamida Barbariyya au Maghribiyya binti Swaaid, huitwa Ummul-Waladu au (Muswafaat).

Kuzaliwa kwake: Siku ya Jumamosi au Jumapili mwezi (7) Safar mwaka (128) hijiriyya.

Sehemu alipo zaliwa: Abwaau, katikati ya mji wa Maka na Madina karibu na Juhfah.

Umri wake: Miaka (55).

Muda wa uimamu wake: Ni miaka (35) kuanzia mwezi (25) Shawwal mwaka wa (148) hijiriyya hadi (25) Rajabu mwaka wa (183).

Nakshi ya pete yake: Hasbiya Llahu, kua na tahadhari kwa Mwenyezi Mungu.

Wake zake: Miongoni mwa wake zake ni Tuktam (Twahirah) na kuniya yake ni Ummul-Banina.

Kifo chake: Mwezi (25) Rajabu mwaka wa (183) hijiriyya.

Sababu ya kifo chake: Alipewa sumu na Haruna Abbasi wakati wa utawala wake baada ya kumuweka jela kwa muda mrefu.

Sehemu aliyo zikwa: Mji mtukufu wa Kadhimiyya, upande wa magharibi ya Bagdad/ Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: