Atabatu Abbasiyya tukufu imetaja mkakati wake wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona ambao imeanza kuutekeleza tangu yalipo tangazwa maambukizi ya virusi hivyo.
Kikosi maalum cha kupambana na maambukizi ya virusi hivyo kilicho undwa na Atabatu Abbasiyya kinaendelea kupuliza dawa sehemu mbalimbali ndani na nje ya Ataba, pamoja na eneo la mji mkongwe na sehemu ya katikati ya haram mbili tukufu, sambamba na kushiriki katika opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika mji mtukufu wa Karbala.
Kuhusu utowaji wa elimu, kazi inayo fanywa kwa kiasi kikubwa na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya, tumesha chapisha na kusambaza maelfu ya vipeperushi, pamoja na kuandaa vipindi vinavyo rushwa kwenye mtandao wa habari wa kimataifa Alkafeel, pamoja na harakati zingine tofauti za kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona zilizo anza mara tu baada ya kutangazwa maambukizi ya virusi hivyo hapa Iraq.
Harakati zote zinafanywa chini ya utekelezaji wa maagizo ya Marjaa Dini mkuu, na mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona katika mji wa Karbala.