Muhimu: Opresheni ya kupambana na Korona.. Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, wakati huu wa amri ya kutotembea kwa ajili ya kupambana na virusi vya Korona, aidha ameongea uwezekano wa kutumia mali ya hazina ya kisheria katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, chini ya kanuni za kifiqhi.

Amewataka wafanya biashara wasipandeshe bei sambamba na kuwataka vijana wajitolee kubaini watu wenye kipato kidogo na kuwapelekea misaada, baada ya kuwasiliana na kamati maalum inayo wajibika wakati huu wa marufuku ya kutotembea.

Amewataka wenye mawakibu Husseiniyya walio jitolea kusaidia wapiganaji kila walicho hitaji wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh, wajitokeze kusaidia familia za wahanga wa maradhi haya.

Ameyasema hayo katika jibu la Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani kufuatia swali lililotumwa ofisini kwake.

Angalia picha iliyo ambatana na habari hii kuona jibu kamili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: