Muhimu: Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza opresheni ya (Marjaiyya Takaaful)

Maoni katika picha
Katika kufanyia kazi wito wa Marjaa Dini mkuu, Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha opresheni iitwayo (Marjaiyya Takaaful) ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo, kutokana na kuwepo kwa marufuku ya kutotembea kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Korona sehemu kubwa ya miji ya Iraq.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Maitham Zaidi amesema kua: “Katika kufanyika kazi wito wa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani wa kusaidia watu wenye kipato kidogo katika jamii, Atabatu Abbasiyya imeanzisha opresheni iitwayo (Marjaiyya Takaaful)”.

Akaongeza kua: Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetoa wito kwa vitengo vyake vyote katika mkoa wa Karbala pamoja na mikoa mingine, ikiwemo idara ya ustawi wa jamii na kikundi cha Alwafaa, na vikundi vinavyo fungamana na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, zikiwepo taasisi za kiraia ziendeshe program za kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo”.

Akasema: “Ataba tukufu imekitaka kikundi cha kutoa huduma katika kikosi cha Abbasi kisaidie kazi ya kusambaza misaada kwa wahitaji katika mkoa wa Karbala pamoja na mikoa mingine”.

Wakatoa wito kwa watu wahisani kusaidia opresheni hiyo katika mikoa tofauti, wakasema hivi karibuni yatatolewa maelekezo ya kuwasiliana na taasisi pamoja na vikundi vya watoa misaada walio chini ya Ataba tukufu.

Tambua kua Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, katika kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: