Marjaa Dini mkuu: Wahisani wanaweza kuhesabu misaada yao kwa familia za masikini katika wanacho kitoa miongoni mwa haki za kisheria

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa wito kwa watu wenye uwezo wa mali kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo katika kipindi hiki cha marufuku ya kutotembea kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya Korona hapa Iraq, akasema kua wanaweza kuhesabu wanacho kitoa katika mali za kisheria, sambamba na kufuata kanuni za kisheria katika ugawaji.

Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Hussein Sistani kufuatia swali lililoulizwa katika ofisi yake.

Lifuatalo ni tamko la jibu lake kuhusu swala hilo:

(Kila mtu mwenye uwezo wa kiuchumi anatakiwa asaidie kulingana na uwezo wake, anaweza kuhesabu anachokitoa katika haki za kisheria, pamoja na kufuata kanuni za kisheria katika ugawaji wake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: