Marjaa Dini mkuu: Wafanya biashara wanatakiwa kuuza bidhaa bila kupandisha bei bali inafaa wapunguze bei

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amewataka wafanya biashara za nafaka za chakula wasizuwie nafaka hizo tena wauze kwa punguzo la bei, kutokana na hali ambayo taifa linapitia kwa sasa, ambapo kunazuwio la kutembea kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya Korona katika miji mingi ya Iraq.

Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatu Llahi Sayyid Ali Husseini Sistani kufuatia swali lililoulizwa katika ofisi yake.

Lifuatalo ni tamko la jibu lake kuhusu swala hilo:

(Wafanya biashara wa nafaka za chakula wasipandishe bei, bali wanatakiwa wauze kwa bei nafuu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: