Marjaa Dini mkuu: Vijana wanatakiwa wasaidie kubaini familia za watu wenye kipato kidogo na wasaidie kuwapelekea nafaka za chakula kwa kushirikiana na kamati maalum inayo husika na marufuku ya kutembea.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amewataka vijana wajitolee kubaini familia za watu wenye kipato kidogo na wasaidie kuwapelekea nafaka za chakula, kwa kushirikiana na kamati maalum inayo husika na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona katika miji mingi ya Iraq, kwa kufuata tahadhari zote zinazo takiwa kujilinda na maambukizi.

Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Hussein Sistani kufuatia swali lililoulizwa katika ofisi yake.

Lifuatalo ni tamko la jibu lake kuhusu swala hilo:

(Vijana wanatakiwa wajitolea kubaini familia za watu wenye kipato kidogo, na wasaidie kuwafikishia misaada ya nafaka za chakula kwa kushirikiana na kamati maalum inayo husika na marufuku ya kutembea iliyopo katika miji mingi ya Iraq kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, lazima wachukue tahadhari zote za kujikinga na maambukizi hayo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: