Marjaa Dini mkuu ametoa wito kwa mawakibu Husseiniyya zilizo simama imara kusaidia wapiganaji wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh, wasaidie familia zitakazo athirika na katazo la kutembea lililo tolewa katika miji mingi ya Iraq kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Akasisitiza kua harakati hizo zifanywe kwa kushirikiana na kamati maalum inayo husika na katazo la kutembea ili kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi.
Lifuatalo ni tamko la jibu lake kuhusu swala hilo:
(Wahudumu wa vikundi vya Husseiniyya –waliosimama imara kusaidia wapiganaji wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh- wanatakiwa wasaidie familia za watu wenye kipato kidogo wanao athirika na katazo la kutembea kwa sasa pamoja na kuzingatia tahathari zoto za kujikinga na maambukizi).