Mwezi ishirini na saba Rajabu ni siku ya kutumwa nuru na kuzaliwa kwa Utume

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na saba Rajabu ni siku ya kukumbuka kupewa Utume kwa Mtume mtukufu, nayo ni miongoni mwa siku tukufu sana, ni siku ambayo ulianza utume, hakika kutumilizwa kwa Mtume (s.a.w.w) ni kutumilizwa kwa nuru na kuzaliwa kwa Quráni tukufu, aidha ni mwanzo wa jamii ya kiislamu, pia hiyo ni siku kubwa, sio ya waislamu peke yao bali binaadamu wote, kutumilizwa kwa Mtume (s.a.w.w) baraka zake zilisambaa kwa viumbe wote.

Mtume (s.a.w.w) alipewa ujumbe wa kiislamu miaka (13) kabla ya kuhama Maka kwenda Madina (Hijra), Mwenyezi Mungu mtukufu alimshushia wahyi kupitia malaika Jibrilu (a.s) kuwa yeye ni Mtume wa binaadamu na mwisho wa mitume.

Hakika kushushwa kwa wahyi na kutumwa Mtume (s.a.w.w) lilikua jambo gumu kwa makafiri, lilikua jambo gumu kwao kifikra na kiimani, kuhusu waumini hawakushangazwa na kushuka kwa wahyi, nafsi zao zilikua zinaamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na ujio wa Mtume kwa ajili ya kuwatoa wanaadamu katika uovu na upotevu, kwani Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanaadamu bila malengo wala hukumuacha bila utaratibu, na akatumia wahyi kua njia ya kujitambulisha kwa mwanaadamu na kumuaongoza katika mambo ya duniani na akhera, pamoja na kuamiliana na watu katika jamii.

Mwenyezi Mungu alimuandaa Mtume wake (s.a.w.w) kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa kiislamu na kuwaokoa walimwengu katika upotevu na ujinga, alipo fikisha miaka arubaini Mwenyezi Mungu alimteua kuwa Mtume wake na akamfanya kuwa sawa na taa lenye mwanga.

Mtume (s.a.w.w) alipokaribia miaka arubaini alianza kupata wahyi kwa njia ya ilhamu na ndoto za kweli ambazo ni miongoni mwa daraja la utume, kisha Mwenyezi Mungu mtukufu akapenda kumtenga na watu, akawa anaenda kukaa katika pango peke yake na kufanya ibada pamoja na kutafakari ukuu wa Mwenyezi Mungu na uumbaji wake.

Kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) anasema: (Alitumwa wakati ambao watu walikua wamezama kwenye upotevu, akahutubia kipindi cha fitina, watu walikuwa wametawaliwa na matamanio, wamepambwa na kiburi, ujinga umewajaa, hawana msimamo wa mambo, Mtume (s.a.w.w) akawapa nasaha, akalingania kwa hekima na mawaidha mema).

Hakika kumbukumbu hii tukufu inatutaka kutafakari historia yake (s.a.w.w), namna alivyo lingania uislamu na kumpwekesha Mwenyezi Mungu mtukufu, ili tuweze kujifunza katika hatua zote za uhai wetu hususan kipindi tulichonacho, tutajifunza mambo mengi yenye manufaa..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: