Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia ofisi yake katika mkoa wa Diyala, imetangaza opresheni ya kusaidia familia zenye kipato kidogo (Marjaiyyatu-Takaaful) kwenye kipindi hiki cha matatizo, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia familia hizo.
Kiongozi wa idara Sayyid Hassan Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Tangu zilipo anza kuchukuliwa tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, miongoni mwa tahadhari hizo ni marufuku ya kutembea, ambayo imeathiri familia za mafakiri ambao kula kwao kunategemea watembee kila siku, tulikua tunafanya kazi za aina mbili, kwanza tumekua tukishirikiana na serikali kupuliza dawa, pili kusaidia familia zenye maisha magumu, kwa kuwapa vitu mbalimbali vinavyo saidia kupunguza ugumu wa maisha katika kipindi hiki.
Akaongeza kua: “Maukibu ya Imamu Hussein (a.s) katika mtaa mpya chini ya idara yetu, ni miongoni mwa mawakibu za kwanza kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, wahudumu wa maukibu hiyo wamegawa vikapu vya chakula kwa familia za watu wenye kipato kidogo baada ya kuwatambua, ugawaji huo unafanywa katika kituo cha maukibu au kwa kuwafuata wahitaji majumbani mwao, kwa namna ambayo inalinda heshima ya familia hizo”.
Akasisitiza kua: Opresheni hii itaendelea katika mawakibu zingine zilizo chini yetu, tunatarajia kushuhudia ongezeko la misaada hiyo katika siku zijazo baada ya agizo la Marjaa Dini mkuu ambalo limetutia moyo na kutupa nguvu zaidi.
Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu ametoa wito kwa watu wote kuunganisha nguvu, katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, kwenye kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo.