Marjaa Dini mkuu: Atakaeambukizwa virusi vya Korona kwa sababu ya akaacha kuchukua tahadhari za kujikinga hatakua na utetezi kisheria

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kua takaeambukizwa virusu vya Korona kwa kuchanganyika na watu -wenye maambukizi- ambao anatakiwa ajitenge nao, yeye akaacha kuchukua tahadhari za kujikinga kisha akaambukizwa hatakua na utetezi kisheria.

Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, kufuatia maswali yaliyotumwa ofisini kwake.

Lifuatalo ni swali na jibu lake kuhusu jambo hilo:

Swali: Hivi ni lazima kuacha kugusana na watu –wenye maambukizi ya Korona- kwa kupeana mikono, kukumbatiana, kubusu na mfano wa hayo, je inafaa kukaa nao bila kuchukua tahadhari za kujikinga kama vile kuvaa barakoa (maski) na tahadhari zingine?

Jibu: (Mtu anae virusi vya Korona kuthofia kuambukizwa virusi vya Korona kwa kuchanganyika na watu wenye maambukizi ya virusi hivyo, ni lazima ajitenge nao. Au akaenao kwa kufuata taratibu zote za kujikinga na maambukizi –kama vile kuvaa barakoa na tahadhari zingine za kidaktari- ambazo anahakika zinamkinga na maambukizi, kama hatachukua tahadhari ya kujikinga halafu akaambukizwa hatakua na utetezi wowote kisheria).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: