Marjaa Dini mkuu: Haifai mwenye maambukizi ya virusi vya Korona kuchanganyika na watu wenyine.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kua haifai kwa mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Korona kuchanganyika na watu wengine, iwapo akichanganyika nao na kusababisha maambukizi kwa mtu mwingine atabeba dhima ya maambukizi hayo, ikitokea aliye muambukiza akifa, muambukizaji atatakiwa kulipa fidia.

Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani kufuatia maswali yaliyotumwa ofisini kwake.

Lifuatalo ni swali na jibu kuhusu swala hilo:

Swali: Mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Korona, je inafaa kuchanganyika na watu wengine wasio jua hali yake ya afya? Akifanya hivyo na ikawa sababu ya kuwaambukiza anakua na hukumu gani kisheria?

Jibu: (Mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Koroni hatakiwi kuchanganyika na watu wengine pale ambapo kuchanganyika huko itakua sababu ya kuwaambukiza, kama akichanganyika nao kisha akawaambukiza atawajibika kwa maambukizi hayo, iwapo aliye ambukizwa atakufa, muambukizaji atatakiwa kulipa fidia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: