Marjaa Dini mkuu ametoa maelekezo kadhaa katika mazingira haya magumu

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa maelekezo kadhaa katika mazingira haya magumu ambayo waumini wanapambana na balaa hili hatari, yapo katika jibu lake Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani alipokua akijibu maswali yaliyoulizwa katika ofisi yake.

Lifuatalo ni swali na jibu kuhusu swala hilo:

Swali: Unausia nini katika mazingira haya magumu ambayo waumini wanapitia kwa sasa kutokana na maradhi haya hatari?

Jibu: (Tunawahusia waumini watukufu mambo yafuatayo):

  • a- Kurejea kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kumuomba aondoe balaa hili, na kuongeza kufanya mema, kama vile kutoa sadaka kwa mafakiri, kusaidia wanyonge, kusoma Quráni tukufu, kusoma dua zilizo pokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s).
  • b- Tunatakiwa kuchukua tahadhari zote zinazo takiwa bila kudharau wala kupuuza, kufuata njia za kujikinga kwa ukamilifu kama zinavyo elekezwa na wataalam wa afya.
  • c- Kutoa elimu kwa watu wengine kuhusu hatari ya virusi vya Korona, na kuwahimiza kuheshimu maelekezo yanayotolewa na idara ya afya.
  • d- Kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo kutokana na kuathiriwa na kusimama kazi kwa sababu ya amri ya kutotembea.
  • e- Kusaidia watu walioambukizwa bila kuangalia dini wala madhehebu zao, na kuwapa kila wanacho hitaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: