Idara ya ustawi wa jamii imetandaza kua; mawakibu zake zimeanza kutekeleza opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful)

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya Shekh Abbasi A’kaaish ametangaza kuwa mawakibu zilizo chini ya idara yake katika mikoa tofauti ya Iraq, zimeitikia wito wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani wa kusaidia familia zenye kipato kidogo katika kipindi hiki kigumu ambacho kuna marufuku ya kutembea katika miji mingi ya Iraq kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Akaongeza kua: “Mawakibu za kutoa misaada katika mkoa wa Basra, Baabil, Diyala, Swalahu-Dini, Misaan na Dhiqaar zimeanza kazi ya kuzibaini familia za watu wenye kipato kidogo katika maeneo yao, chini ya kanuni na maelekezo ya idara ya afya na kamati inayo simamia marufuku ya kutembea”.

Akasisitiza kua: “Kuna mawakibu nyingi tayali zimesha anza kutoa misaada ya chakula na mahitaji mengine ya familia hizo”.

Akasema kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu siku zijazo tutashuhudia ongezeko la mawakibu na maeneo yanayopewa huduma”.

Tambua kua Marjaa Dini mkuu ametoa wito kwa mawakibu za kutoa misaada zilizo kua na mchango mkubwa katika kusaidia wapiganaji wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh, zisaidie familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo katika mazingira haya magumu ambayo kuna marufuku ya kutembea kwenye miji mingi ya Iraq kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: