Mawakibu Husseiniyya zimeanza opresheni kubwa ya kusaidia wenye shida kipindi hiki cha virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Hussiniyya katika Ataba mhili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetangaza opresheni kubwa ya mawakibu Husseiniyya zilizo chini yake kwenye mikoa tofauti, ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo katika kipindi hiki kigumu, ikiwa ni kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia familia hizo.

Rais wa kitengo bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mawakibu za Husseiniyya zimeanza kutoa misaada kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ambao wameathirika na hatua zinazo chukuliwa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, wameanza opresheni hiyo tangu lilipo tolewa agizo na Marjaa Dini mkuu, huo ndio utaratibu wa mawakibu wakati wa mitihani mikubwa, ukiwemo mtihani wa magaidi wa Daesh, walitoa mchango mkubwa katika kufanikisha ushindi dhidi ya magaidi hao na kukomboa taifa la Iraq”.

Idara ya mawakibu katika mkoa wa Basra ni moja na vituo vya opresheni hiyo, mawakibu zilizo chini yake kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wao bwana Basam Shahmani wameanza opresheni waliyo ipa jina la (Ihna-Mamnuniin), ambayo ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kugawa chakula kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ambao wameathiriwa na katazo la kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Akaongeza kua: “Tumeunda kamati inayofanya kazi ya kubaini familia za wahitaji na sehemu walipo pamoja na kuwapelekea mahitaji yao, wataendelea na kazi hadi wazifikie familia zote tulizo zisajili, na kuhakikisha misaada hiyo inapunguza ugumu wa maisha wakati huu wa mtihani”.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kuungana katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ndio Atabatu Abbasiyya ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: