Zaidi ya familia 1200 zimefikiwa na wawakilishi wa kikosi cha Abbasi katika mikoa tofauti ndani ya siku mbili zilizo pita

Maoni katika picha
Kupitia opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) iliyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya na kutekelezwa na wawakilishi wa kikosi cha Abbasi kwenye mikoa tofauti hapa Iraq, tayali zaidi ya familia (1200) za watu wenye kipato kidogo zimefikiwa ndani ya siku mbili katika kipindi hiki ambacho kuna marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Wawakilishi wa kikosi wamezifikia familia hizo katika mkoa wa Muthanna, Waasit, Misaan sambamba na kugawa vipeperushi vinavyo elezea namna ya kujikinga na virusi vya Korona.

Wakati huohuo tunaendelea na kazi ya kubaini familia zinazo hitaji kusaidiwa chakula, pamoja na kuwasiliana na wahusika kwa ajili ya kurahisisha utendaji.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kuungana katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ndio Atabatu Abbasiyya ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: