Katika opresheni ya kupambana na Korona: Maktaba ya Atabatu Abbasiyya imeanzisha huduma ya kuazima vitabu ukiwa mbali

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na Korona, imeanzisha huduma ya kuazima vitabu ukiwa mbali, huduma hiyo inatolewa bure hadi zitakapo isha tahadhari za kiafya.

Kupitia huduma hiyo mdau wa maktaba anaweza kuazima kwa njia ya mtandao hadi vitabu vinne ndani ya wiki moja.

Masharti na madhumuni ya huduma hii:

  • 1- Walengwa wa huduma hii ni wanafunzi wa elimu za juu wanaosoma kwenye vyuo vikuu vya Iraq, kwa sharti la kutuma vitambulisho vya chuo unacho soma.
  • 2- Unaweza kuazima mara moja kwa wiki.
  • 3- Mnufaika atasajiliwa kupitia anuani yake ya barua pepe, hivyo ni lazima iwe inafanya kazi.
  • 4- Maombi yeyote yenye upungufu hayatashughulikiwa au yatakayo kua na taarifa zinazo pingana na ukweli.
  • 5- Utajibiwa kulingana na maombi yako, tunaomba muwe na subira na muwe waelewa.
  • 6- Kabla ya kujaza fomu, andika namba ya maombi na kitabu unacho hitaji kwa rangi ya kijani, kwenye mtandao wa maktaba kupitia link ifuatayo”

https://www.alkafeel.net/library/elec_lib/

Zingatia:

  • - Kuwepo kwa alama ya (*) mbele ya kolam inamaanisha kua hiyo kolam ni ya lazima.
  • - Ili ombi lako lishughulikiwe.. lazima ufuate masharti ya uombaji na uzingatie maelekezo yaliyopo mbele ya kila kolam na yale yaliyopo ndani ya mabano.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa (library@alkafeel.net) au piga simu namba (009647806088899).

Kwa mahitaji ya vitabu vya kwenye mtandao ingia katika nink ifuatayo:

https://forms.gle/ua35GhvfWtjnGMNf8
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: