Opresheni kubwa ya kupuliza dawa theluthi mbili za mji mtukufu wa Karbala

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kupitia shughuli kubwa ya kupuliza dawa, wanayo itekeleza kwa kushirikiana na serikali, idara za utumishi na mwezi mwekundu, kinatarajia kupuliza dawa theluthi mbili za mkoa mtukufu wa Karbala.

Kamanda wa kikosi cha usafi katika kituo cha jeshi la wananchi Saádi Ismaili amesema kua: “Tayali tumesha puliza dawa maeneo ya katikati ya mji, Ainu-Tamru, Husseiniyya, Hindiyya na mitaa yote ya makazi ya watu na sehemu za biashara, sasa hivi tunaendelea kupuliza dawa katika mtaa wa Nasru/13 na 14 kisha tutaelekea katika mtaa wa Swamadu, kazi itaendelea hadi maambukizi ya Korona yatakapo isha”. Akatoa wito kwa wananchi wazingatie marufuku ya kutembea na wafuate maelekezo ya wizara ya afya kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi.

Kiongozi wa jumuiya ya mwezi mwekundu tawi la Karbala bwana Mustafa Waathiqu Salmaan, amesema kua: Imebaki sehemu ndogo kumaliza kupuliza dawa ya kupambana na maambukizi ya Korona, na kulinda usalama wa wananchi kutokana na maradhi hayo, akasema: “Shughuli hii imeenda pamoja na kuwajengea uwezo wananchi kuhusu hatari za ugonjwa huo na namna za kujikinga nao”.

Wananchi wamepongeza kazi hii na wamekishukuru kikosi cha wapiganaji cha Abbasi, ambacho ni mashuhuri kwa ujemedari wao wa kulinda taifa, na leo kimesimama imara kupambana na adui mwingine ambaye ni kirusi, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awatie nguvu watekelezaji wa mradi huu waendelee kufanya kazi hiyo kwa faida ya taifa na dunia kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: