Atabatu Abbasiyya yakanusha kuambukizwa mtumishi wake yeyote virusi vya Korona

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umekanusha habari za kuambukizwa virusi vya Korona mmoja wa wafanyakazi wake, habari ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii, wamesisitiza kua hakuna mtumishi yeyote aliye ambukizwa virusi hivyo.

Wakasema kua wao wamechukua hatua zote za kujikinga na virusi hivyo, kupitia kamati maalum iliyo undwa, na bado wanaendelea kufanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara za afya, kazi ya kupuliza dawa bado inaendelea tena kwa umakini mkubwa.

Wametoa wito kwa wananchi kuchukua taarifa zinazo husu Atabatu Abbasiyya kutoka kwenye vyanzo vyake vya habari.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imefanya mambo mengi ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, na inafanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya, katika ngazi ya Ataba, mji na mkoa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: