Katika kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu kupitia opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) inayafanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, mawakibu zilizo chini ya idara ya ustawi wa jamii zinaendelea kugawa misaada usiku na mchana kwa familia zilizo athiriwa na marufuku ya kutembea, ofisi ya mkoa wa Basra ni sawa na ofisi za mikoa mingine, inaendelea kufanya kazi ya kugawa chakula na vitu vingine kwa familia zenye uhitaji.
Ofisi hiyo kupitia mawakibu zilizo chini yake imekusanya vitu kutoka kwa wahisani na kuandaa msafara wa (Marjaiyyatu-Takaaful) kwenda kugawa misaada kwa mafakiri na familia za watu wenye kipato kidogo, ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea iliyo tolewa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, msafara huo umegawa aina tofauti za vyakula, kwa ajili ya kupunguza ugumu wa maisha kwa familia hizo.
Washiriki wa msafara huo wamesema kua wataendelea na opresheni hiyo katika miji mingine hadi hali hii itakapo isha, wanufaika wa misaada hiyo wamepongeza na kushukuru namna Marjaa Dini mkuu anavyo wajali, sawa na mzazi kwa watoto wake, na wakawashukuru sana walio ratibu misaada hii.