Kikosi cha Abbasi katika mkoa wa Karbala chakaribisha mradi wa Marjaiyyatu-Takaaful wa kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimepokea kwa furaha mradi wa Marjaiyyatu-Takaaful, ulio anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, ambao wamekua wahanga wa marukufu ya kutembea iliyo wekwa kwenye miji mingi ya Iraq, na kuathiri maisha yao kutokana na kutegemea kutembea kila siku ili wapate riziki yao.

Kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa kikosi hicho, tayali wanazihudumia familia za wahitaji katika mitaa mitatu ndani ya mkoa wa Karbala, katika hatua ya kwanza wametoa vikapu vya chakula (150) kwa kila mtaa.

Akabainisha kua: Utambuzi wa familia zenye uhitaja umefanywa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maeneo hayo, kwa kutumia kamati maalum itakayo endelea kusaidia mawasiliano nao hata kama jambo hili litachukua muda mrefu –Allah atuepushie- kikosi kinafanya juhudi kubwa ya kujaza chakula katika maghala yake kwa ajili ya kujiandaa na ukame wowote unaoweza kutokea, sambamba na kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Tambua kua kikosi kimeshatoa matangazo ya kupokea misaada na kuigawa kwa wahitaji.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kushirikiana katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ndipo Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha mradi wa Marjaiyyatu-Takaaful kwa ajili ya kusaidia watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: