Kwa kuzaliwa Imamu Hussein (a.s) limewaka taa la uongofu

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi tatu Shabani mwaka wa nne Hijiriyya katika mji wa Madina, alizaliwa Imamu Hussein (a.s) ndani ya nyumba ya utume na kituo cha malaika, akalelewa chini ya uangalizi wa babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) na walii wa Mwenyezi Mungu baba yake Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) na mama yake mtoto wa mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa mtoto wa Muhammad (s.a.w.w).

Mtume Muhammad (a.s.w.w) alikua na umakini maalum kuhusu Imamu Hussein, unao onyesha umuhimu wake tangu akiwa mdogo, Mtume (s.a.w.w) alikua anahusia kuwapenda maimamu wawili Hassan na Hussein (a.s), alisema: Atakaempenda Hassan na Hussein nitampenda, na nitakaempenda Mwenyezi Mungu atampenda, atakaependwa na Mwenyezi Mungu ataingizwa peponi, na atakae wachukia nitamchukia, na atakaechukiwa na mimi atachukiwa na Mwenyezi Mungu, na atakaechukiwa na Mwenyezi Mungu atakaa motoni milele), akasema tena (s.a.w.w): (Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussein, anapendwa na Mwenyezi Mungu mwenye kumpenda Hussein, Hussein ni miongoni mwa wajukuu wangu).

Wakati wa kuzaliwa Imamu Hussein karama nyingi zilionekana, nataja baadhi yake:

Namna alivyo pewa jina Imamu Hussein (a.s): Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimuuliza Imamu Ali (a.s): (Umempa jina gani mwanangu?), Imamu Ali (a.s) akamjibu: (Siwezi kukutangulia kumpa jina ewe Mtume wa Mwenezi Mungu), Mwenyezi Mungu akamshushia wahyi Mtume (s.a.w.w) akamtajia jina la mtoto huyo, Mtume (s.a.w.w) akamuangalia Imamu Ali (a.s) halafu akamuambia: (Mwite Hussein).

Mtume wa Mwenyezi Mungu alimrithisha ukarimu wake na akamfanya kua muendelezaji wa wahyi wake na malengo yake.

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) alikua anawalinda wajukuu zake wasifikwe na baya lolote, Ibun Abbasi anasimulia kua: Mtume (s.a.w.w) alikua anawalinda Hassan na Hussein kwa kusema: (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yote kutokana na kila shetani na kila jicho baya) kisha anasema: (Hivi ndio alivyokua Ibrahim akiwalinda watoto wake Ismaili na Is-haqa).

Abdurahmaan bun Aufu anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) aliniambia: (Ewe Abdu Rahmaan nikufundishe maneno ya kujilinda; maneno ambayo Ibrahim alikua anawalinda watoto wake Ismaili na Is-haqa na mimi nayatumia kuwalinda watoto wangu Hassan na Hussein, Mwenyezi Mungu anatosha kua mlinzi kwa mwenye kumuomba wala hakuna siraha inayo zidi amri ya Mwenyezi Mungu), mapenzi na upole wake kwao yalionyesha wazi kilele cha namna alivyokua anawajali, alikua anawalinda dhidi ya ubaya wowote wala hakutaka wadhurike na vijicho au husda.

Imamu Hussein (a.s) alikua anafanana na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kimaumbile na kitabia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: