Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kila mwaka linapo chomoza jua la kujitolea, katika kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s) mwezi tatu Shabani, hubeba mauwa kutoka katika haram tukufu ya Abbasi hadi kwenye kaburi lake takatifu, na hufurahi pamoja na waumini wengine kutoka kila kona ya dunia.
Hupokewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya, kwa pamoja huweka mauwa juu ya kaburi takatifu, na hunyanyua mikono yao juu chini ya kubba tukufu, mahala ambapo Imamu Swadiq (a.s) anasema dua hukubaliwa, wamemuomba Mwenyezi Mungu aondoe balaa katika nchi yetu kipenzi na nchi zingine zote duniani, wakiwa wamefuata maagizo yote ya kujikinga na maambukizi ya maradhi ya Korona.
Hivyo ndio wanavyo fanya waumini wote katika siku hii tukufu, iwe kukubaliwa dua kwao sawa na zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika kumbukumbu hii, na kuburudisha macho yao kwa kuangalia kubba mbili kwa karibu wakiwa kwenye eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imeshafanya mambo mengi kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, imeunda kamati maalum kwa ajili ya kupambana na virusi hivyo, inafuata maelekezo yote yanayo tolewa na idara ya afya, katika kiwango cha Ataba na majengo yake au mji mkongwe, ikiwa ni pamoja na kuzuwia mikusanyiko na kuahirisha swala za jamaa pamoja na kusimamisha baadhi ya harakati zake za kielimu na kitamaduni.