Mwezi nne Shabani dunia iliangaziwa kwa kuzaliwa mwezi wa bani Hashim

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi nne Shabani ni kumbukumbu ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s) anayeitwa Mwezi wa bani Hashim, kwa kuzaliwa kwake dunia ilingára na nuru ikaangaza, alinyonya maziwa ya ushujaa na kulelewa na miguu ya ukhalifa.

Historia ya kuzaliwa kwake (a.s): Abulfadhil Abbasi (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina, mwezi nne Shabani mwaka wa ishirini na sita hijiriyya.

Hakika mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s) amezaliwa mwezi mmoja na ndugu yake Imamu Hussein (a.s) wametofautiana siku moja tu, aidha kuna tofauti ya miaka ishirini na tatu tangu kuzaliwa kwa Imamu Hussein hadi alipozaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s), alikua mtoto wa kwanza wa Ummul-Banina, Madina ilitikisika na kunawirika kwa kuzaliwa kwake, furaha ikaingia ndani ya familia ya Alawiyya, umezaliwa mwezi wao amboa unaangazia mbingu ya dunia, na umeongeza utukufu wa bani Hashim.

Kiongozi wa waumini alipopewa taarifa za kuzaliwa mtoto huyo mtukufu, alikwenda nyumbani haraka akambeba na kumbusu, akamfanyia mambo ya kisheria ya watoto, akamuadhinia katika sikio la kulia na kumkimia katika sikio la kushoto, sauti ya kwanza aliyo sikia ilikua ni sauti ya baba yake, isemayo (Allahu Akbaru…) (Laa ilaaha-illa llah).

Siku ya saba toka kuzaliwa kwake Abulfadhil Abbasi (a.s), kiongozi wa waumini (a.s) akamnyoa nywele, na akatoa sadaka ya dhahabu au fedha kwa uzito wa nywele hizo, akawapa masikini kisha akamchinjia mbuzi wa hakika, kama alivyo wafanyia ndugu zake Hassan na Hussein (a.s) kama alivyo elekeza Mtume (s.a.w.w).

Kupewa kwake jina: kiongozi wa waumini (a.s) alimpa mwanae jina la (Abbasi), alikua anajua kua atakua jemedari wa kiislamu, atakua chukizo kwa waovu na wapenda batili, na furahisho kwa wapenda kheri, alikua kama alivyo bashiriwa, hakika alikua jemedari katika uwanja wa vita, aliteketeza makamanda wa uovu, alikua tishio kwa maadui wote katika vita ya Karbala.

Tambua: alikua na sura nzuri sana, aliitwa mwezi wa bani Hashim kutokana na uzuri wake, alikua mkamilifu wa maumbile alama za ushujaa zilionekana katika mwili wake, alikua mrefu kiasi anaweza kupanda juu ya farasi na miguu yake ikiwa imeganyaga chini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: