Kwa video: Kupambwa dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mauwa katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Maoni katika picha
Mwezi nne Shabani ni siku aliyozaliwa Abbasi bun Ali bun Abu Twalib (a.s) ajulikanae kwa jina la Mwezi wa bani Hashim.

Masayyid wanaofanya kazi katika malalo yake takatifu wamelipamba dirisha takatifu kwa mauwa katika siku hii tukufu aliyo zaliwa jemedari wa vita ya Twafu, mtu aliyekua na umuhimu wa pekee kwa Imamu Hussein (a.s), baada ya tukio hilo majukumu yoto yakabakia kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s), ikawa kama vile kubakia kwake hai ni sehemu ya ukamilifu wa uaminifu wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hakika Abulfadhil Abbasi (a.s) ni mtukufu na mtu wa pekee, yatosha kua fahari kwake pale Imamu Hussein (a.s) alipo muambia (Panda kwa ajili yangu ewe ndugu yangu), na pale alipo mkinga kwa nafsi yake yote hayo yanaonyesha wazi utukufu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: