Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amesema kua Ataba tukufu itajenga kituo cha kupokea watu walioambukizwa virusi vya Korona katika opresheni yake ya kujikinga na virusi vivyo.
Akaongeza kua: “Tunafanya hivyo chini ya maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kutokana na umuhimu wa kushirikiana katika kupambana na tatizo la dunia kwa sasa na kwa upande mwingine tatizo la taifa letu kipenzi, kazi hiyo itafanywa chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya (ujenzi wa kituo kitakacho pokea watu walioambukizwa virusi vya Korona) pembeni ya hospitali kuu ya Hindiyya, kama sehemu ya kupambana na virusi hivyo”.
Kiongozi wa idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya Dokta Osama Abdu-Hassan amesema kua: Kituo kitakachojengwa na Atabatu Abbasiyya katika hospitali kuu ya Hindiyya ni kwa ajili ya watu walioambukizwa virusi vya Korona, baada ya tatizo hili kuisha kitaendelea kutoa huduma za afya, kwani jengo hilo litakua sehemu ya majengo ya hospitali, linajengwa kama sehemu ya upanuzi wa hospitali hiyo.
Akaongeza kua: “Mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala pamoja na idara ya hospitali ya Hindiyya kama wanufaika wa mradi, tayali tumesha fanya vikao vilivyo husisha idara ya madaktari na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya, na tumekubaliana kujenga vyumba 32 vya wagonjwa vitakavyo kua na kila kitu cha lazima pamoja na vyumba 6 vya madaktari”.
Akasema: “Hicho ni kituo maalum kwa ajili ya watu walioambukizwa virusi vya Korona na kitajengwa na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, chini ya usimamiza wa hospitali ya rufaa Alkafeel na idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Kumbuka kua watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi wamesha anza kazi ya kujenga vituo vya kutoa huduma kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Ataba na hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kujiandaa na kukabiliana na tatizo hili kama likitokea –Allah atuepushie- pia ni maandalizi ya kupokea wagonjwa hao.
Mradi huo ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia sekta ya afya, chini ya mkakati wa kulinda jamii na maambukizi ya virusi vya Korona.