Mwezi tano Shabani iliangaza nuru ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi tano Shabani mwaka wa 38 hijiriyya alizaliwa Imamu Sajjaad Zainul-Aabidina (a.s), aliye kua kisima cha elimu na hekima duniani, historia yake ni mfano mkubwa kwa watu namna alivyo ipa nyongo dunia na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Aliishi na babu yake kiongozi wa waumini (a.s) miaka miwili, na akaishi na Ammi yake Hassan miaka kumi, na pamoja na baba yake Hussein (a.s) miaka kumi na moja, baada ya kifo cha baba yake akaishi miaka thelathini na nne, alifia katika mji wa Madina mwaka wa tisini na tano hijiriyya, akiwa na umri wa miaka hamsini na saba.

Mama yake ni Shahribanuyah bint wa Shahriyari bun Kisra, anaitwa pia Shaha Zanaan, kiongozi wa waumini alimwita Maryam, na inasemekana alimwita Fatuma, aidha inasemekana kua alimuhusia Imamu Hussein kua: “Mfanyie wema Shahribanuyah hakika karidhiwa atakuzalia mbora wa watu wa duniani baada yako”. Katika tukio lingine akasema kua “Yeye ni mama wa mawasii wa kizazi kitakasifu”.

Kuzaliwa kwake: Siku aliyo zaliwa (a.s) babu yake kiongozi wa waumini na baba yake Imamu Hussein (a.s) walifanya haraka kutekeleza wajibu wa kisheria kwa mtoto, aliadhiniwa katika sikio la kulia na akasomewa iqama kwenye sikio la kushoto ukawa ni msingi wa uchamungu katika moyo wake, ukawa ni mwangi uliodumu katika maisha yake yote uliomuongoza kwenye wema.

Kitu cha kwanza alicho sikia Imamu Zainul-Aabidina katika dunia hii ilikua ni sauti isemayo (Allahu Akbaru) iliyokaa katika moyo yake, siku ya saba akachinjiwa hakika na akakatwa nywele halafu ikatolewa sadaka ya dhahabu au fedha kwa uzito wa nywele zake kwa masikini, kama ilivyo agizwa na Mtume (s.a.w.w).

Laqabu zake (a.s): Zainul-Aabidina, Sajjaad, Mwenye sugu, Mwingi wa kulia, Al-Aabidu na mashuhuri zaidi ni Zainul-Aabidina, imepokewa kutoka kwa Zuhuri kua alikua anasema: “Kuna sauti itaita siku ya kiyama, asimame pambo la waabudio katika zama zake, atasimama Ali bun Hussein (a.s), na aliitwa mwenye sugu (dhu Thaqnaat) kwa sababu viungo vya sajda vilikua na sugu kutokana na wingi wa kusujudu kwake”.

Kuhusu laqabu ya Mwingi wa kulia, imepokewa kutoka kwa Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) kua: Ali bun Hussein alimlilia baba yake miaka ishirini, ndani ya miaka hiyo kila kilipowekwa chakula mbele yake alilia, baadhi ya wafuasi wake walikua wanamuambia: ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunaogopa usije ukaangamia.

Naye alikua anasema: Hakika nashitakia huzuni yangu kwa Mwenyezi Mungu na ninajua msiyo yajua, sijataja mauwaji aliyo fanyiwa baba yangu na ndugu zangu na watoto wa Ammi zangu ispokua huchomwa na mwiba kooni kwangu.

Amani iwe juu ya Zainul-Aabidina na burudisho la macho ya watazamaji siku aliyo zaliwa na siku aliyo uwawa na siku atakayo fufuliwa kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: