Opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika majengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kikosi cha kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza kazi ya kupuliza dawa sehemu zote zinazo tumika kupokea mazuwaru watukufu kwa ajili ya kuwalinda na maambukizi ya virusi vya Korona.

Msimamizi wa kazi hiyo Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua kazi hii tulianza kuifanya tangu siku za nyuma na bado tunaendelea kuifanya chini ya ratiba maalum iliyo pangwa na kamati ya kujikinga na maambukizi, ambayo ni kuendelea kupuliza dawa majengo yate ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kua: “Tunatumia vifaa kazi maalum ambavyo Ataba imepewa na shirika la Khairul-Juud vinavyo endana na mazingira ya majengo hayo, sehumu zinazo pulizwa dawa ni kumbi zote, vyumba, vyoo, korido, kuta za ndani na nje pamoja na njia zote zinazo elekea kwenye majengo hayo”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inafanya opresheni maalum ya kupuliza dawa maeneo yote yanayo zunguka Ataba pamoja na mji mkongwe na barabara zote zinazo elekea Ataba, kama sehemu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: