Siku 6 za kufanya kazi mfululizo saa 24: watumishi wa Atabatu Abbasiyya wamefikia hatua za mwisho katika mradi wa ujenzi wa kituo cha wagonjwa wa Korona

Maoni katika picha
Kazi mfululizo saa 24 ndani ya siku 6, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kitengo cha usimamizi wa kihandisi wamefanya kazi ya kujenga kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona kama nyuki bila kukaa wala kupumzika, kituo ambacho kitakua sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, siku baada ya siku jengo linaanza kuonyesha muonekano wake.

Mhandisi bwana Ammaar Swaleh mahdi ameuamba mtandao wa Alkafeel hatua waliyo fikia kwa sasa: “Kazi ya ujenzi wa kituo inaenda kama ilivyo pangwa, tunatarajia kumaliza kwa wakati, miongoni mwa kazi zilizo kamilika katika hatua ya kwanza ni:

  • - Tumemaliza ujenzi wa boma la chuma pamoja na uwekaji wa (Sandwitch panel).
  • - Kuanza hatua za umaliziaji katika:
  • 1- Ufungaji wa (jipsam bod) umekamilika kwa asilimia %70.
  • 2- Ufungaji wa nyaya za umeme umekamilika kwa asilimia %20.
  • 3- Uwekaji wa marumaru umekamilika kwa asilimia %80.
  • 4- Uwekaji wa matundu ya vyoo pamoja na viambata vyake umekamilika kwa asilimia %40 na tumesha weka sinki 15 upande wa mashariki.

Sehemu ya pili inayo enda sambamba na sehemu ya kwnza maendeleo yake ni:

  • - Ufungaji wa boma la juma umekamilika kwa asilimia %90.
  • - Ufungaji wa sandwitch panel umekamilika kwa asilimia %70”.

Akasisitiza kua: “Kazi zote zinaendelea vizuri mfululizo saa 24 kwa siku, huku wafanya kazi wakiwa na zamu tatu, asubuhi, mchana na usiku, wanafanya kazi bila kusimama”.

Tambua kua kazi hii ni utekelezaji wa agizo la Marjaa Dini mkuu la kusaidia sekta ya afya, pia ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kupambana na virusi vya Korona, ndipo mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya na kufuatia maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba hiyo Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi wakaanza ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) ndani ya mkoa mtukufu wa Karbala, chini ya usimamizi wa kamati ya madaktari ya Ataba na hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kujiandaa na tatizo hilo –Alla atuepushie-, pamoja na kuandaa kumbi maalum za kupokea watu wenye matatizo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: