Katika kusaidia sekta ya elimu kwenye mazingira ya sasa: Kituo cha kukuza vipaji Alkafeel kimeweka punguzo la %86 katika App ya Siraji

Maoni katika picha
Kituo cha kukuza vipaji Alkafeel kimetangaza punguzo la asilimia %86 kwenye App yake ya Siraji kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika mazingira haya magumu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona hapa Iraq.

Kiongozi wa kituo Ustadh Samiri Swafi amesema kua: “Punguzo hili linatokana na hali ngumu ambayo taifa linapitia kwa sasa, kutokana na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ambayo pia imepelekea kufungwa kwa shule”.

Akaongeza kua: App ya Siraji iliyo anzishwa baada ya kukusanya maoni ya walimu na kua kiunganishi kati ya shule na mwanafunzi pamoja na wazazi, App hiyo ni nzuri sana hasa wakati huu mgumu ambao taifa linapitia kwa sasa.

Akabainisha kua: App ya Siraji inaweza kutumiwa na mwalimu au mzazi pamoja na mwanafunzi kwa kutumia simu za kisasa (smart phone) zenye uwezo wa (Android) na (IOS) kupitia intanet.

Akafafanua kua: “Kwa kutumia App hiyo unaweza kupokea masomo kutoka kwa walimu kwa namna tofauti na viwango tofauti, pia unaweza kukutana na wanafunzi pamoja na walimu tofauti”.

Kwa maelezo zaidi tembelea link ifuatayo:

http://www.school.iq

Au piga simu namba (07810206373) au tuma barua kupitia barua pepe: info@school.iq
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: