Mhandisi bwana Ammaar Swalahu Mahdi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeongeza eneo la (2m250) kwenye mradi, ambazo hazikuwepo kwenye ramani ya kwanza, mafundi wameanza kujenga boma la chuma na wanatarajiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda mfupi”.
Akabainisha kua: “Baada ya kuingia hatua ya tano inayo husisha umaliziaji wa shughuli za mradi, tumeongeza nguvu kazi hadi kufikia asilimia %200”.
Akafafanua kua: “Katika hatua ya tano tumefanya mambo yafuatayo:
- Kuweka viyoyozi katika vyumba vya wagonjwa na kumbi.
- Kufunga nyaya za umeme.
- Ujenzi wa vyoo na viambata vyake.
- Kuweka maji vyooni.
- Kupaka rangi.
- Kukata sehemu zingine kwa kutumia Jipsam bodi.
- Kufanya upanuzi kwa ajili ya mradi mpya”.
Akasisitiza kua: “Kazi zote zinaendelea vizuri na zinafanywa saa 24, wafanyakazi wamepangiwa zamu tatu, asubuhi, mchana na usiku, kazi zinaendelea bila kusimama hata kidogo”.
Kumbuka kua mradi huu ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, ndipo mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wakaanza kazi hii chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi wa kujenga kutuo hiki katika mji wa Imamu Hussein (a.s) ndani ya mkoa wa Karbala, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Ataba tukufu na hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kujiandaa na tatizo hilo –Alla atuepushie-, pamoja na kuandaa kumbi maalum za kupokea watu wenye maambukizi ya virusi vya Korona.