Katibu mkuu wa Ataba tukufu anakagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar, alasiri ya Jumanne (6 Shabani 1441h) sawa na (31 Machi 2020m) amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona akiongozana na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, kituo ambacho kitakua sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa mtukufu wa Karbala.
Katibu mkuu amesema kua: “Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia sekta ya afya nchini, pamoja na maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba Sayyid Ahmadi Swafi, ya kujenga kituo chenye sifa zinazo hitajiwa na wanufaika, kituo hiki ni msaada kwa hospitali na sehemu salama kwa wagonjwa na familia zao”.
Akaongeza kua: “Mradi huu ni sehemu ya msaada wa Ataba tukufu kwa taifa katika sekta ya afya, msaada wa kwanza ulikua ni kugawa barakoa (maski) kutoka shirika la Khairul-Juud na kupuliza dawa sehemu za makazi ya watu pamoja na kugawa baadhi ya vifaa tiba”.
Akabainisha kua: “Ziara yetu katika mradi huu unaotekelezwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi ni kwa ajili ya kuangalia utendaji ambao umefikia hatua nzuri kutokana na juhudi kubwa za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaofanya kazi saa (24), hii ndio desturi yao katika utendaji hasa inapokua kazi ni ya kujitolea kwa ajili ya kuhudumia jamii, utawakuta wanashindana katika kufanya kazi”.
Mwanachama wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema kua: “Mradi huu ni sehemu ya juhudi za kupambana na virusi vya Korona vinavyo sumbua dunia kwa sasa, leo kamati kuu ya uongozi wa Ataba tukufu ikiongozwa na katibu mkuu pamoja na makamo wake wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huu ambao umekamilika kwa kiwango kikubwa”.
Kumbuka kua mradi huu ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, ndipo mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wakaanza kazi hii chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi wa kujenga kituo hiki katika mji wa Imamu Hussein (a.s) ndani ya mkoa wa Karbala, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Ataba tukufu na hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kujiandaa na tatizo hilo –Alla atuepushie-, pamoja na kuandaa kumbi maalum za kupokea watu wenye maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: