Shirika la Khairul-Juud limetangaza bidhaa mpya zitakazo ingizwa katika matumizi hivi karibuni

Maoni katika picha
Shirika la Khairul-Juud linatarajia kutoa bidhaa mpya za kujikinga na kujisafisha wiki ijayo, katika mkakati wa kijikinga na maambukizi ya virusi vya korona, bidhaa hizo ni soksi za kuvaa mikononi.

Mkuu wa shirika hilo Ustadh Maitham Bahadeli ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunapenda kuwapa moyo wananchi watukufu, hususan wanao tumia bidhaa za shirika la Khairul-Juud, kiwanda kinafanya kazi saa 24 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya soko ya vifaa vya kujikinga na visafishio”.

Akaongeza kua: “Bidhaa zinazo tengenezwa na shirika letu ni salama kwa mtumiaji na rafiki kwa mazingira, zinaubora mkubwa na viwango vya kimataifa, bidhaa mpya zitauzwa bie nafuu na zitakua na ubora mkubwa”.

Tambua kua shirika la Khairul-Juud lilikua limesha tangaza kuongeza uzalishaji wa vifaa vya kujikinga na visafishio, kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji mara tano zaidi, ili kuwapatia wananchi na vituo vya afya vya Karbala na kwenye mikoa mingine kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: