Eneo lililo ongezwa katika kituo cha kuhudumia watu wenye maambukizi ya virusi vya Korona limefikia hatua za mwisho ndani ya saa 24

Maoni katika picha
Eneo lililo ongezwa katika kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, lenye ukubwa wa (2m250) limefikia hatua za mwisho ndani ya saa (24), kazi zote za hatua ya tano zinaendelea vizuri.

Mhandisi bwana Swalahu Mahdi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi kuongeza utendaji wake hadi asilimia %200, kazi za hatua ya tano ambayo ndio hatua ya mwisho zinaendelea vizuri.

Akaongeza kua: “Sehemu iliyo ongezwa haikuwa katika ramani ya mradi hapo awali, jengo hilo litakua sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa mtukufu wa Karbala, upo katika hatua za mwisho baada ya kuongeza utendaji hadi asilimia %200”.

Kumbuka kua wanufaika wameomba kuongeza eneo lenye ukubwa wa (2m250) kwenye mradi, eneo hilo halikuwepo kwenye ramani ya kwanza, ambapo litajengwa sehemu za madaktari na kumbi za kutolea huduma pamoja na eneo la vyoo, mafundi wameanza kujenga boma la chuma tangu jana asubuhi na wanatarajia kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda mfupi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: