Kutanduliwa asilimia (90) ya mazulia katika haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kila baada ya msimu watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya hutandua mazulia yaliyopo na kutandika mengine au kuacha wazi baadhi ya sehemu zilizo kua zimetandikwa kwa ajili ya kudumisha mazingira ya usafi.

Katika kufanyia kazi utaratibu huo tayali asilimia (90) ya mazulia yametanduliwa ndani ya haram tukufu, kazi hii imeenda sambamba na shughuli za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zinazo fanywa na kamati maalum iliyo undwa na Ataba tukufu.

Makamo rais wa kitengo Ustadh Zainul-Aabidina Adnani Ahmadi Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi ya kubadilisha mazulia hufanywa kila baada ya muda fulani, hua tunabadilisha pamoja na kufanya usafi sanjari na kupuliza manukato ndani ya haram, mwaka huu kazi hii imesadifu shughuli za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zinazo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (kinga ni bora kuliko tiba)".

Akaongeza kua: “Mazulia yaliyo baki ambayo ni asilimia (10) yametandikwa sehemu maalum zisizokua za wazi ndani ya haram tukufu”.

Akasisitiza kua: “Mazulia hubadilishwa kila baada ya siku tatu, kisha huoshwa na kupulizia dawa kabla ya kutandikwa tena, tulikua tunafanya hivyo toka zamani lakini tumeongeza usafi zaidi baada ya kutokea balaa hili la virusi vya Korona”.

Kumbuka kua shughuli hii ni sehemu ya opresheni inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kazi ya usafi hufanywa kila siku na kipindi cha kiangazi hubadilishwa mazulia yote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: