Katika kufanyia kazi maagizo na maelekezo ya wizara ya elimu ya juu, chuo kikuu cha Alkafeel kimeanza kufundisha kwa njia ya masafa (UIMS), chini ya ratiba ya masomo ya chuo kwa ubora mkubwa na kwa kuzingatia uwezo wa intanet, aidha njia hii inamrahisishia mwanafunzi kuwasiliana na mwalimu wake.
Tumeongea na ustadh Ali Hassan kiongozi wa idara ya utendaji katika chuo amesema kua: “Njia hii (UIMS) inamuwezesha mwanafunzi kupata masomo kwa namna mbalimbali, kwa nakala za maandishi, picha na video, pia anaweza kufanya mitihani akiwa mbali (kwa njia ya masafa) pamoja na kupata majibu ya mitihani yake kwa njia hiyohiyo, hali kadhalika mwalimu anaweza kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, njia hii inamfanya mwanafunzi aendelee na masomo akiwa nyumbani kwao”.
Akaongeza kua: “Hakika mfumo huu ulianza kutumiwa na chuo tangu miaka miwili iliyo pita, katika kutoa maelekezo muhimu na ratiba za masomo ya kila wiki pamoja na ratiba za mitihani, baada ya maelekezo ya mkuu wa chuo, tumeboresha mtandao chini ya usimamizi na msaada wa mkuu wa taaluma, jopo la wataalam wetu limeongeza vipengele kwenye mfumo huo ili kumuwezesha mwanafunzi kuendelea na masomo akiwa nyumbani kwao”.
Akasisitiza kua: “Mfumo huu unafanya kazi kwenye kompyuta mbalimbali na simu ganja (smart phone) zenye uwezo wa (Android) na (Ios)”.
Kumbuka kua chuo kimeanza kutumia mfumo huu kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo wakiwa majumbani kwao, sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona kwa usalama wao.