Kikosi cha Abbasi kinaendelea kupuliza dawa katika mji mtukufu wa Karbala

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea kupuliza dawa katika mji mtukufu wa Karbala chini ya mkakati wa Hashdi Shaábi katika mkoa huo.

Msemaji wa kikosi cha Abbasi ameripoti kua, maeneo yaliyo pulizwa dawa ni pamoja na mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad) kuelekea barabara ya Hauraa upande wa kaskazini na katikati ya mji pamoja na barabara ya Jamhuri.

Akasema kua jumla ya gari 14 zilizo beba tenki zenye ukubwa tofauti zimeshiriki katika zowezi hilo, na wapiganaji 40 waliobeba tenki za dawa migongoni wamepuliza dawa sehemu ambazo gari haziwezi kuingia, karibu lita 5000 za dawa zimetumika.

Tambua kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kwa kushirikiana na shirika la Khairul-Juud, walianza kazi ya kupuliza dawa katika mkoa mtukufu wa Karbala siku ya tarehe (16 Machi 2020m) na bado wanaendea hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: