Viyoyozi vimekamilika kwa asilimia (100) katika kituo cha kuhudumia watu wenye maambukizi ya Korona

Maoni katika picha
Mhandisi bwana Ammaar Swalahu Mahdi ametangaza kua ufungaji wa viyoyozi katika kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kituo ambacho kitakua sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, umekamilika kwa asilimia (100).

Akaongeza kua: “Tumefunga zaidi ya viyoyozi 70 vyenye ukubwa tofauti, katika vyumba vya wagonjwa, kumbi za kutolea huduma na vyumba vya madaktari”.

Akabainisha kua: “Kazi hii imefanywa ndani ya muda mfupi, nayo ni sehemu muhimu katika hatua ya tano ya umaliziaji”.

Akasisitiza kua: “Hakika ufungaji wa viyoyozi umefanywa na Ataba tukufu katika mradi huu”.

Kumbuka kua mafundi wanaofanya kazi kwenye kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, walianza ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala na katika hospitali kuu ya Hindiyya, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari ya Ataba tukufu na hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kujiandaa kukabiliana na janga hili –Allah atuepushie-.

Pia mradi huu ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia sekta ya afya, chini ya program ya kulinda jamii na maambukizi ya virusi vya Korona.

Aidha Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) ya kusaidia familia zenye kipato kidogo, baada ya Marjaa Dini mkuu kutoa wito wa kuungana katika kusaidia familia hizo wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: