Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/ 26 Hashdi Shaábi) kinasaidia wizara ya kilimo katika mkoa wa Muthannah, kupambana na nzige waliopo kwenye jangwa la Samawah, kama wasipo dhibitiwa mapewa wanaweza kuleta maafa makubwa sana na wataendelea kuongezeka.
Kiongozi wa usalama kwenye kikosi hicho, Ustadh Maahir Abdulhassan amesema kua: “Tulipokea maombi kutoka idara ya kilimo katika mkoa wa Muthanna ya kwenda kupambana na nzige waliovamia kwenye jangwa na mkoa huo, na kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) tumetuma kikosi tulicho kipa kazi mbili, kwanza ni kupuliza dawa kwenye vidongoji mbalimbali vya Samawah vilivyo ainishwa awali, pili ni kushirikiana na wizara ya kilimo katika kuwapulizia dawa nzige waliovamia jangwa la Samawah kwa kutumia vifaa mbalimbali zikiwemo na ndege zisizokua na rubani”.
Kumbuka kua makundi makubwa ya nzige yamevamia jangwa la Samawa katika eneo la (Inswaab) karibu na mtaa wa (Baswiyah), nzige hao wamefunika eneo lenye ukubwa wa kilometa 100, na wamekua hatari kubwa katika mashamba.
Hali kadhalika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) bado kinaendelea kushirikiana na jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala kubuliza dawa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, katika wakati huu wa marufuku ya kutembea.