Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya anakagua maendeleo ya kazi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi leo siku ya Jumamosi mwezi (10 Shabani 1441h) sawa na tarehe (4 Aprili 2020m), ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, unaojengwa katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala.

Mheshimiwa amefuatana na makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi na kitendo cha usimamizi wa kihandisi ambao ndio watekelezaji wa mradi, amekagua maendeleo ya kazi na kusikiliza maelezo kutoka kwa watendaji.

Kiongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s) Dokta Swabahu Husseini amesema kua: Ufuatiliaji binafsi wa Mheshimiwa Sayyid Swafi katika mradi huu unatia moyo sana, mradi huu umekuja wakati muwafaka, tulikua na haja kubwa ya mradi wa aina hii, utakapo kamilika utaweza kulaza wagonjwa (60) kila mmoja akiwa kwenye chumba cha peke yake.

Akabainisha kua: “Miradi hii inahitaji muda mrefu kukamilisha vigezo vya kidaktari vinavyo hitajika, lakini watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu siku chache zijazo watakamilisha na kukabidhi mradi ukiwa tayali kutoa huduma kwa wagonjwa”.

Kumbuka kua mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia walio ambukizwa virusu vya Korona, unajengwa kama zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel kwa mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, na walio chukua jukumu la ujenzi wa kituo hiki ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: